Luke 22:47-52

47 aIsa alipokuwa bado anazungumza, umati mkubwa wa watu ukaja. Uliongozwa na Yuda, ambaye alikuwa mmoja wa wale wanafunzi Kumi na Wawili. Akamkaribia Isa ili ambusu. 48Lakini Isa akamwambia, “Yuda, je, unamsaliti Mwana wa Adamu kwa busu?”

49Wafuasi wa Isa walipoona yale yaliyokuwa yanakaribia kutokea, wakasema, “Bwana, tuwakatekate kwa panga zetu?” 50 bMmoja wao akampiga mtumishi wa kuhani mkuu kwa upanga, akamkata sikio la kuume.

51Lakini Isa akasema, “Acheni!” Akaligusa lile sikio la yule mtu na kumponya.

52 cKisha Isa akawaambia wale viongozi wa makuhani, maafisa wa walinzi wa Hekalu, pamoja na wazee waliokuwa wamekuja kumkamata, “Mmekuja na panga na marungu, kana kwamba mimi ni mnyang’anyi?
Copyright information for SwhKC